Subaru


Subaru ni kampuni ya Kijapani inayotengeneza magari aina ya Subaru na vifaa mbalimbali. Inajulikana hasa kwa utengenezaji wa magari aina ya Legacy, Forester, Impreza na mengineyo. Subaru ni kampuni mashuhuri duniani kwa sababu wanatengeneza magari yanayosukuma tairi zote na kutumia injini bapa inayofanya kazi kama mpigana ngumi. Subaru ilibadilisha jina kutoka 'Fuji Heavy Industries Ltd' mnamo mwaka 2017 na kuitwa 'Subaru Corporation' jina hili lilitokana na brand ya magari yao ambalo lilikua maarufu zaidi kuliko jina la kampuni yenyewe kwa muda huo.

Asili ya neno Subaru ni 'Nakajima' ambayo ni kampuni ya ndege iliyoanzishwa na bwana Chikuhei Nakajima mwaka 1917. Baada ya vita vya pili vya dunia Nakajima ilijikita katika utengenezaji wa vyuma mbalimbali ikitumia teknolojia ya utengenezaji wa ndege, na baiskeli. Mnamo mwaka 1945 kampuni hii ilivunjwa na kutenganishwa katika vipande vitano ambavyo baadae viliungana na kuunda kampuni ya 'Fuji Heavy Industries' mwaka 1953.

Ngao ya Subaru ina nyota ndogo tano na moja kubwa. Hii inamaanisha yale makampuni matano yaliyoungna pamoja na kutengeneza kampuni moja kubwa. Neno Subaru linamaanisha kikundi cha nyota za 'Plaides' au kukusanyika pamoja kwa kijapani.

Mwaka 2005 kampuni ya Toyota ilinunua hisa kutoka Subaru na kuifanya kuwa mmiliki mkubwa, hata hivyo haikuimeza kampuni ya Subaru yote bali iliiacha iendelee kama kampuni huru katika uzalishaji wake wa magari.

Magari ya Subaru  yamekua yakipata ufaulu mkubwa kwenye tathmini ya usalama, kuna ucheshi unaosema 'Watu wa uokozi hawayapendi magari ya subaru kwa sababu yanachukua sana muda kuyakata baada ya ajali kwa sababu yana miamba migumu'. Hii ni kweli kwani watu wengi wanatoka salama kwenye ajali za subaru tofauti na magari mengine.

Subaru inajulikana sana kama watengenezaji wa injini bapa(flat) zinazofanya kazi kama mpigana ndondi/ngumi(boxer). Kwa sasa ni kampuni za Subaru na porsche tu wanaotumia mfumo huu wa injini ambao mara nyingi hutumiwa kwenye injini za ndege na garimoshi.

Watu wengi wanaifahamu subaru kama gari ya mashindano, lakini Subaru illingia kwenye mashindano ya magari mwaka 1989 ilipoungana na Prodrive ya uingereza kutumia Subaru Legacy RS. Subaru imeshinda mara sita taji la 'World Rally Championship' miaka ya 1995,1996,1997, 2001 na 2003. Hadi sasa subaru ni kampuni pekee iliyoshiriki mashindano hayo kwa muda mrefu zaidi. Ila mwaka 2008 Subaru ilitangaza kujitoa katika mashindano haya kwani ilishakamilisha nia yake ya kujitangaza.

Tofauti na Toyota, kampuni ya Subaru haijajiimarisha sana barani Africa, kwani inawawakilishi katika nchi chache tu ikiwemo Misri, Kenya na Afrika kusini, lakini hali hii haijawazuia watu kutoka nchi nyingine kuagiza magari yao.

Nchini Tanzania kabla ya mwaka 2010 magari ya Subaru hayakuwa yakifahamika ni watu wachache sana waliokuwa nayo. Soko lilimilikiwa na Toyota kwa asilimia zaidi ya 90%, watu waliyaogopa sana kwa sababu waliamini kuwa yanakula sana mafuta pia upatikanaji wa spea ulikua mgumu. Hali imebadilika kwa sasa kwani watu wamezidi kununua magari haya baada ya upatikanaji wa spea kua rahisi.

Tanzania hakuna muwakilishi rasmi wa Subaru ila kampuni huru kama hii ya Fuji zimekua zikitoa huduma bora na msaada wa urekebishaji kwa wateja na wamiliki wa magari ya subaru.

Kwa maoni na msaada wa kiufundi au mengineyo kuhusiana na gari lako la Subaru usisite kututafuta kupitia email au namba zetu za simu.