Matatizo ya Subaru


Matatizo Makuu ya Subaru

Subaru kama magari mengine ina matatizo machache yanayorekebishika ambayo hujitokeza mara kwa mara kutokana na utengenezaji kutoka kiwandani au hali ya matumizi ya mtu binafsi. Matatizo haya hujumuisha

Kuvujisha na Kuchoma Oil

Kuvuja kwa oil kwenye magari aina ya subaru husababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo na kubaribika kwa 'Head gasket'

'Head Gasket' ni kifaa maalumu kinachotumika kuunganisha vipande viwili tofauti vya injini ili kuziba nafasi na kuzuia upenyaji wa oil na coolant kwenda nje. Kifaa hichi kanapo haribika husababisha injini kuvuja oil na coolant hivyo hupelekea vimiminka hivyo kupungua na kusababisha hali ya hatari kwenye injini.

Sio injini zote za subaru hupatwa na matatizo haya, kuna makundi mawili ya injini zenye hatari kubwa ya kupata tatizo hili. Kundi la kwanza ni injini za lita 2.5 za kizazi cha kwanza za mwaka 1996 hadi 1999 zilizoumika kwenye modeli za Outback, Legacy na Impreza R.S., katika kundi hili head gasket huanza kuvuja ndani kwa ndani na mwisho wake husababisha injini kuchemsha.

Dalili za kwaza za kufeli kwa head gasket kwenye kundi la kwanza ni kutokea kwa mabaki ya oil/mafuta kwenye tenki la coolant na kwenye mfumo wa exhaust, pia kutakua na harufu ya mafuta na sulfur kenye tenki la coolant.

Kundi la pili ni injini za kizazi cha pili za lita 2.2 na 2.5 zinazopatikana katika Forester na Impreza za mwaka 1998 na Legacy za 2000. Dalili za kwanza katika kundi hili ni uvujaji wa oil na coolant unaaonekana kwa nje karibu na head gasket yenyewe.

Kugonga kwa Steering za Umeme(EPS)

EPS ni mfumo wa kundeshea gari unaotumia mota ya umeme badala ya hydraulic katika ukataji wa kona. Mfumo huu katika Subaru ulianza kutumika kwenye magari ya automatic kuanzia miaka ya 2008 kuja juu. Mfumo huu unafaida kwani hautaji nguvu nyingi kucontrol gari pia hupunguza ulaji wa mafuta ukilinganisha na wa hydraulic ambao hutumia pump inayosukumwa na injini.

Kwa modeli hizi za kwanza, gari inapopita kwenye makorongo kwa muda mrefu husababisha 'seal' zilizopo ndani ya 'steering rack' kuchoka na kuanza kugonga na kutetemeka.

Tatizo hili linarekebishwa kwa kubadilisha au kuzibana 'seal' ndani ya rack ili kutoa mitetemeko, pia watu wengine huamua kubadili mfumo mzima wa steering kutoka wa umeme kuja wa hydraulic ili kukomesha kabisa tatizo hili.

Tags: subaru