Bei ya Subaru Forester Tanzania
Magari ya Subaru yameendelea kupata umaarufu zaidi nchini Tanzania miaka ya hivi karibuni, ikionekana watu wengi zaidi hasa vijana wakipendelea kuyaagiza. Hii inathibitishwa kwa kushika nafasi ya pili na ya sita katika magari maarufu yanayoagizwa kupitia kampuni za Beforward na Sbtjapan ikizipita Toyota Rumion, Harrier, Spacio na Nissan Juke.
Hapo zamani magari aina ya Subaru yalikua adimu kupatikana Tanzania, watu wengi waliyaogopa kutokana na ukosefu wa 'spare parts' vilevile magari haya yalihusishwa na magari ya mbio (racing cars) hivyo watu waliamini kuwa yanakula mafuta sana. Kwa mkoa wa Arusha hali ilikua tofauti kwani ukilinganisha na mikoa mingine Subaru ilikua maarufu kwa miaka mingi sana huko, hii ilisababishwa na kuwepo jirani na nchi ya Kenya. Kenya wamekua watumiaji wa Subaru kwa miaka mingi zaidi hadi kupeleka kuwa na official Subaru dealer nchini kwao, hii imesababisha upatikanaji wa 'spare' na 'service' kuwa rahisi kwa kipindi kirefu ukilinganisha na Tanzania.
Hali kwa sasa imebadilika,ingawa soko la Tanzania bado linashikwa na Toyota kwa asimilia 80%, kwa zaidi ya miaka tano au sita sasa uingizaji wa magari ya Subaru umeongezeka kwa kasi sana na kupelekea kushika soko kwa asimilia 3% baada ya Nissani yenye asilimia 4%. Ongezeko hili lilisababishwa na watu kugundua kuwa magari aina ya Subaru ni ya kawaida na yanauzwa kwa bei ya chini ukilinganisha na modeli sawa za Toyota. Kwa mfano mwaka 2016-2018 bei ya Subaru Forester 2008 uliweza kuipata kwa shilingi millioni 19 wakati Harrier 240G ilikua millioni 22 hadi 24 wakati huo. Kwa sasa bei zimepanda kutokana na wahitaji(demand) kuongezeka.
Fuji Heavy Garages ni kampuni ya Kitanzania ya urekebishaji wa magari ambayo kwa sasa imebobea zaidi kwenye magari aina ya Subaru, kwa msaada na ushauri wa bure kabla na baada ya kununua gari lako la Subaru unaweza kututafuta kwa kutumia mawasiliano haya.
Bei za Subaru Forester 2022
Forester ni mojawapo ya modeli za magari yanayotengenezwa na Subaru yenye muundo wa SUV, modeli hii ni maarufu zaidi ukilinganisha na nyingine kwa sababu ni kubwa na inafaa kwa matumizi ya familia. Bei hutegemeana na mwaka wa uzalishaji, hadi sasa kuna vizazi(generations) vitano vya uzalishaji wa gari hili kutokea mwaka 1997 lilipoanza kutengenezwa, hivi hujumuisha
Toleo la Kwaza (SF) 1997 - 2002
Soko | No. Usajili | Bei | Usafiri | Ushuru (TRA) | Clearance | Jumla |
---|---|---|---|---|---|---|
Nje/Agiza | NA | Tsh 7,000,000 - 8,000,000 | Tsh 3,172,000 | Tsh 5,757,307.37 | Tsh 1,500,000 | Tsh 16,000,000 - 18,000,000 |
Ndani | A** | Tsh 7,000,000 - 8,000,000 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 7,000,000 - 8,000,000 |
B** | Tsh 7,000,000 - 10,000,000 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 7,000,000 - 10,000,000 | |
C** | Tsh 7,500,000 - 10,500,000 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 7,500,000 - 10,500,000 | |
D** | Tsh 8,000,000 - 16,000,000 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 8,000,000 - 16,000,000 |
Toleo la Pili (SG) 2002
Soko | No. Usajili | Bei | Usafiri | Ushuru (TRA) | Clearance | Jumla |
---|---|---|---|---|---|---|
Nje/Agiza | NA | Tsh 3,500,000 - 4,000,000 | Tsh 3,172,000 | Tsh 5,757,307.37 | Tsh 1,500,000 | Tsh 14,000,000 - 16,000,000 |
Ndani | A** | Tsh 7,000,000 - 8,000,000 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 7,000,000 - 8,000,000 |
B** | Tsh 7,000,000 - 10,000,000 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 7,000,000 - 10,000,000 | |
C** | Tsh 7,500,000 - 10,500,000 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 7,500,000 - 10,500,000 | |
D** | Tsh 8,000,000 - 16,000,000 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 8,000,000 - 16,000,000 |
Toleo la Tatu (SH) 2008
Soko | No. Usajili | Bei | Usafiri | Ushuru (TRA) | Clearance | Jumla |
---|---|---|---|---|---|---|
Nje/Agiza | NA | Tsh 6,500,000 - 10,000,000 | Tsh 3,172,000 | Tsh 9,453,955.77 | Tsh 1,500,000 | Tsh 19,000,000 - 30,000,000 |
Ndani | A** | NA | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | NA |
B** | NA | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | NA | |
C** | Tsh 11,500,000 - 15,500,000 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 11,500,000 - 15,500,000 | |
D** | Tsh 15,000,000 - 24,000,000 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 15,000,000 - 24,000,000 |
Toleo la Nne (SJ) 2012
Soko | No. Usajili | Bei | Usafiri | Ushuru (TRA) | Clearance | Jumla |
---|---|---|---|---|---|---|
Nje/Agiza | NA | Tsh 11,500,000 - 30,000,000 | Tsh 3,172,000 | Tsh 12,217,416.66 | Tsh 1,500,000 | Tsh 28,000,000 - 46,000,000 |
Ndani | A** | NA | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | NA |
B** | NA | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | NA | |
C** | NA | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | NA | |
D** | Tsh 27,000,000 - 46,000,000 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 27,000,000 - 46,000,000 |
Toleo la Tano (SK) 2018
Soko | No. Usajili | Bei | Usafiri | Ushuru (TRA) | Clearance | Jumla |
---|---|---|---|---|---|---|
Nje/Agiza | NA | Tsh 46,000,000 - 65,000,000 | Tsh 3,172,000 | Tsh 27,630,741.69 | Tsh 1,500,000 | Tsh 77,000,000 - 96,000,000 |
Ndani | A** | NA | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | NA |
B** | NA | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | NA | |
C** | NA | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | NA | |
D** | NA | Tsh 0 | Tsh 0 | Tsh 0 | NA |